Rappers wa Arusha leo kufanya battle na graffiti

 

Mamc wa Arachuga leo wanakutana pande za Kijenge juu kupiga battle za hatari na mitindo huru.

Wakati wale mamc wakigaragazana kwa mistari, wengine  waliobarikiwa kipaji cha uchoraji watakuwa wakizipiga kuta za jirani kwa graffiti za hatari katika kudumisha msingi mmoja wapo wa hip hop jijini humo.

Issue nzima itafanyika kuanzia saa tisa nje ya studio ya Watengwa.

Hakuna kiingilio bali ni miguu tu ya wapenzi wa hip hop wa Arachuga ikihusika zaidi.

“Amani itawale sana hapo SUA na Mungu awape nguvu mambo yaende salama kabisa!watu wajae kwa wiiiiiiiiingi!wape salama kina,omary roca,daz,ally faza na baba wa ukoo,mo plus!,” ameandika Nash Mc kwa kumweleza JCB aliyetoa tangazo hilo.