Rick Ross aachia single ya tatu kutoka kwenye 'God Forgives I Don’t

 

Rick Ross jana, July 2, ameachia single ya tatu, Hold Me Back kutoka kwenye albam yake mpya God Forgives I Don’t.

 

Ngoma hiyo ambayo imetengenezwa  na producer Rico Love inadaiwa kufanana kidogo na touch za nyimbo alizowahi kutengeneza producer huyo kwenye albam ya kambi ya Rick Ross, Maybach Music Group.

 

Nyimbo hizo ni pamoja na "Actin' Up" uliopo kwenye “Self Made Vol. 2" na"Tupac Back" kutoka kwenye "Self Made Vol. 1."

Albam hiyo ya tano ya Rick Ross inatarajiwa kuingia sokoni July 31 mwaka huu.

 

Single ya kwanza kutoka ilikuwa ni "So Sophisticated" akiwa na Meek Mill ambayo kwa sasa imekamata nafasi ya  99 kwenye chart ya Billboard ya R&B/Hip-Hop Songs, na ya pili ni "Touch N' You" akiwa na Ushe r iliyopo nafasi ya 22.

soundcloud.com/defjam/rick-ross-hold-me-back