Sauti za Busara yanukia, bado siku 7 tu!

Zimekabi siku saba tu hadi lile tamasha kubwa  la muziki barani Afrika la Sauti za Busara lianze. Maandalizi yanaendelea kwenye viwanja vya Ngome Kongwe  visiwani Zanzibar.

Tamasha hili linalokutanisha wasanii mbalimbali kutoka barani Afrika litafanyika kuanzia Feb 14 – 17.

Wasanii watakaotumbuiza mwaka huu ni pamoja na:

Cheikh Lô (Senegal)  Mlimani Park Orchestra (Tanzania)  Khaira Arby (Mali)  Comrade Fatso & Chabvondoka (Zimbabwe)  Culture Musical Club (Zanzibar / Tanzania)  Atongo Zimba (Ghana / UK)  N'Faly Kouyaté (Guinea)  Nathalie Natiembe (Reunion)  Zanzibar Unyago (Zanzibar / Tanzania)  Nawal & Les Femmes de la Lune (Comoros / Mayotte)  Owiny Sigoma Band (Kenya / UK)  Mokoomba (Zimbabwe)  Msafiri Zawose & Sauti Band (Tanzania)  Mani Martin (Rwanda)  Burkina Electric (Burkina Faso / Austria)  Lumumba Theatre (Tanzania)  Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden)  Super Maya Baikoko (Tanzania)  Peter Msechu (Tanzania)  Wakwetu Jazz Vibes (Tanzania)  Safi Theatre Group (Tanzania)  DCMA Young Stars (Zanzibar / Tanzania)  Wanafunzi wa SOS (Zanzibar / Tanzania)  na wengine.