Serengeti, Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro Crater zashinda shindano la maajabu saba ya dunia

Mbuga ya wanyama ya SERENGETI imeshika nafasi ya kwanza katika shindano la maajabu saba ya dunia ya Afrika.

Pamoja na Serengeti, mlima Kilimanjaro na Ngorongoro Crater nazo zimeshinda shindano hilo.

Majina hayo yalitangazwa wiki hii jijini Arusha na Rais wa 'New Seven Wonders,' Dr Philip Imler.

Washindi wengine walikuwa ni 'Red Sea Reef,' mto Nile na Okavango Delta ya Botswana.