Soggy Doggy ashangaa namna watanzania wengi walivyo maskini wa kutupa

 

Baada ya kukaa kwa muda mrefu katika mazingira ya mjini hususan jijini Dar es Salaam, rapper mkongwe nchini Tanzinia, Anselm Ngaiza aka Soggy Doggy, amejionea jinsi upande mwingine wa Tanzania ulivyo katika safari yake ya Mwanza.

Soggy ambaye yupo kwenye ziara ya kimuziki kanda ya ziwa akiwa na wenzake D-Knob na Bwana Misosi walifanikiwa kushuka sehemu na kupiga picha na wananchi wa vijijini.

 

Kupitia Facebook, Soggy ambaye pia ni mtangazaji wa Uhuru Fm amesema:

“Ndugu zangu Watanzania,nchi yetu ina eneo kubwa kuliko mnavyodhania.Wakati mkifanya ufisadi wa kudidimiza nchi kuna sehemu watu hawana huduma muhimu yoyote na hata sura zao zimekubali matokeo..Mungu bariki my motherland.”

 

Kabla ya kuelekea Mwanza wasanii hao walipita mjini Dodoma ambako walikuwa na mwalikobungeni.

Awali Soggy alidai kuwa nia ya ziara hiyo ni kukutana na mashabiki wao ambao hawajawaona kwa muda mrefu kutokana na majukumu yanayowakabili.