TANZANISKA RIKSFÖRBUNDET

CHAMA CHA WATANZANIA SWEDEN (TANZANISKA RIKSFÖRBUNDET)

Kwa Watanzania pamoja na Marafiki!

Kamati ya muda iliyoteuliwa Ubalozini kwa nia ya kuanzisha chama cha watanzania Sweden inawakaribisha katika hafla fupi ya ufunguzi wa chama na pia kuchagua viongozi watakaondeleza shughuli za chama. Mgeni wa Heshima katika ufunguzi na uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Watanzania atakuwa Mh. Balozi Muhammed Mwinyi Haji Mzale.

Sehemu: Tanzania house, Näsby Allè 6, Täby

Tarehe: 28/4/2012

Wakati: Saa Tisa mchana mpaka saa kumi na moja jioni.

Mwaliko utatumwa kwa barua pepe ikiambatanisha fomu za kujiandikisha kugombea uongozi wa chama. Pia waweza kupakua katika tangazo lilowekwa katika mtandao wa Ubalozi. https://www.tanemb.se/index.php?option=com_content&task=view&id=165&Itemid=36

Wote mna karibishwa na ukipata taarifa hii tafadhali mtumie na mwingine!

Kamati ya wanamchakato kupitia

Katibu wa Muda

Bi. Angela Wilberd:

tanzanianswe@hotmail.com