Video Clip Mpya Ya Lord Eyez Akirap Kuhusu Ommy Dimpoz na Majanga

Ni wiki kadhaa zimepita tangu rapper wa Swahili Hip Hop kutoka kundi la WEUSI Lord Eyez kutuhumiwa na mwanamziki wa Bongo Flava Ommy Dimpoz katika sakata la wizi wa vifaa vya gari yake. Tukio ambalo lilimake headline katika vyombo mbalimbali vya habari na kibaya zaidi liliweka doa katika kundi linalopendwa sana kutoka Arachuga Weusi Kampuni. Japokuwa Ommy Dimpoz mwenyewe alishawai sema kwamba yaishe kiroho safi tuu na game liendelee, lakini kesi ya sakata ilo bado inaendelea kwani Lord Eyez ni mtuhumiwa tuu na bado hajakutwa na hatia. 

Tarehe 23 November 2012 Mtayalishaji wa Muziki kutoka Bongo Records P Majani ambae Taifa zima la Tanzania linamkubali nakuamini yeye ndie Legendary katika utayalishaji wa muziki wa Kizazi kipya na ndie aliewatoa wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya amepost kipande kifupi cha video kinachomuonesha Lord Eyez akiwa studio. 

Rapper Huyo mkali ameonekana akirap kwa hisia kali katika beat yenye mdundo wa masikitiko na akizungumza jinsi gani baadhi ya watu wengi wanavyomzushia mambo mengi kuanzia tukio la Ommy Dimpoz na Ray C. Wapenzi wa muziki wa Hip hop watakuwa wanaisubili sana iyo ngoma pindi itakapoisha na uenda ikawa moja kati ya nyimbo kali za funga mwaka kutoka katika studio za Bongo Records. JanB Online itajitahidi kumtafta Lord Eyez na Majani ili kupata habari zaidi kuhusu project hii. Iangalie hii video clip Lord Eyez akichana na kufunguka kwa hisia kali: www.youtube.com/watch?v=U7AR7Npp_Tw //JanB Multimedia