Wasanii watakaotumbuiza kwenye fainali ya kombe la mataifa Afrika watajwa

Michuano ya wiki tatu  ya kombe la mataifa ya Afrika, Orange AFCON,  inayoendelea nchini Afrika Kusini inatarajia kumalizika Jumapili hii kwenye uwanja wa taifa wa nchi hiyo mjini Johannesburg.

Wasanii sita wa Afrika  wametajwa kutumbuiza kwenye fainali hizo ambao ni pamoja na staa wa Nigeria D'Banj, Zonke, Kelly Khumalo na Thembesile Ntaka wa Afrika Kusini, Muthoni wa Kenya na kundi la Micasa.

Sherehe za ufungwaji wa michuano hiyo zitatanguliwa na presentation na performance ya Yvonne Chaka Chaka akiwa kama balozi mwema wa Roll Back Malaria Partnership.

Atasindizikizwa na mchezaji wa zamani Mark Fish atakayetoa hotuba fupi kuhusu Malaria.