Will.i.am amtetea Nicki Minaj kufanya Pop

 

Producer na mwanamuziki wa kundi la Black Eyed Peas Will.i.am amemtetea Nicki Minaj  licha ya kukoselewa na baadhi ya wapenzi wa muziki kutokana na albam yake ya pili Pink Friday: Roman Reloaded.

Licha ya rapper huyo wa Young Money kusisitiza kuwa bado ameendelea kusimama kwenye misingi ya hip hop nyimbo kama 'Starships' zimewafanya mashabiki wake wa ukweli kuamini vinginevyo.

 

 

Mtangazaji wa Hot 97, Peter Rosenberg amewahi kumdiss rapper huyo kwa kuuita wimbo huo "bulls**t."

Will.i.am naye ajikuta katika suala hilo kwa kuambiwa kuwa ameikimbia hip hop hivyo si jambo la kushangaza kumtetea Nicki.

"I am proud of Nicki," aliliambia jarida la Vibe.

"Hip-Hop ilikuwa ikijikuza yenyewe miaka ya ‘90s, sasa hivi hip-hop inajizuia yenyewe. Kama hiphop itaendelea kuwazuia watu basi nasema  ‘F**k hip-hop."

"Namtaka Nicki aendelee kuionesha dunia jinsi Hip-Hop inavyoweza kuwa. Sio lazima iwe kuhusu kumchapa demu huyu ama kupata hela.”